VIONGOZI KUWATAKIA WAISLAMU EID AL-ADHA NJEMA
Written by Inka FM on 20 July 2021
Wakenya wanajumuika na waumini wajamii ya kiislamu kusherehekea eid-al-adha moja ya sherehe katika kalenda ya kiislamu.
Eid al-adha, kiarabu ina maana ya kutoa kafara alivyowajibika abrahamu kumtoa mwanae ishmaeli kama ishara ya kumtii sheria ya mungu.Hata hivyo, Mungu alimpa Abrahamu mwana kondoo ambaye alimchinja badala yake Ishmaeli.
Viongozi wa kisiasa, mashirika tofauti na watu binafsi wamemimina jumbe za heri njema kwa ndugu zetu waislamu wanapoadhimisha sherhe za siku hii ya eid al-adha nchini na kote duniani.
Baadhi ya viongozi hao ni naibu wa rais Dkt William Ruto.Ujumbe wa Ruto kupitia ukrasa wake wa twitter, “We salute the Muslim fraternity around the world as they observe ‘Eid al-Adha. This is the celebration to honor the sacrifice and devotion to God. May this special holy day bring love and inspire us to work for the wellbeing of everyone. Happy ‘Eid al-Adha!”
Ikimbukwe kuwa hiyo jana Ruto akiwa mjini Mombasa aliwanunua mbuzi wa kichinjwa katika sherehe ya leo.
Aliyekuwa waziri mkuu na kiongozi wa ODM Raila Odinga naye andika katika ukurasa wake, “on this ‘Eid al-Adha I would like to wish our Muslim brothers and sisters ‘Eid Mubarak. May you all be blessed and become stronger in your faith whose hallmark is respect and tolerance for all.”
Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi vilvile amewataka waislamu wote washerehekee kwa amani na faraja ya mwenyezi Mungu na kuwarai waiombee nchi yetu huku wakitafakari kafara wanazo zitoa.
Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kwa upande mwingina ameitakia jamii ya kiislamu baraka kabla nabaada ya sherehe za mwaka huu.
Ikumbukwe kwamba sherehe hii ya ‘Eid al-Adha, ni ya kuwachinja wanyama na kwatoa kafara kama ibada, ambapo robo tatu ya nyama hiyo huliwa na familia zinazotoa kafara, inayosalia hupewa maskini na wanaohitaji katika jamii.
Eid Mubarak !